Ifikapo Tusije tukajidanganya kama tusipofanikiwa tutaendelea kwa usalama, kuna hatari ya amani ya nchi na usalama kuvurugika”
Warioba.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Joseph Warioba amewataka viongozi wa vyama vya siasa kukutana na kufikia
makubaliano ili mchakato wa Katiba uendelee hatimaye kupatikana kwa
Katiba Mpya kwa masilahi ya Taifa.
Pia, Jaji Warioba ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu
amemshauri Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein
kuchukua hatua zitakazoondoa matatizo katika Bunge Maalumu la Katiba
ili kuwezesha mchakato huo kukamilika.
Akizungumza katika mahojiano maalumu ofisini kwake
Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema ni muhimu viongozi hao kuweka
kando tofauti zao za mawazo na mitizamo ili kupata Katiba Mpya kwa
masilahi ya taifa.
Warioba ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali
mstaafu, ameonya kwamba ikiwa viongozi hao hawataweka kando tofauti zao
na kuwezesha Taifa kupata Katiba Mpya, amani ya Taifa inaweza
kuvurugika.
“Tunatoa wito kwa viongozi wa vyama wakutane
watafakari hali ilivyo na kufikia makubaliano ili mchakato uendelee.
Tunafikiri ni jambo bora wakarudi na usiwepo mjadala wa kuangalia idadi
ya kura katika kufikia uamuzi, lengo lisiwe idadi ya kura, bali
makubaliano ya kupata Katiba Mpya,” alisema jaji Warioba na kubainisha:
“Kipindi chote, sisi tuliokuwa wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba tulikuwa tukifuatilia kwa karibu sana mchakato
unavyoendelea. Sisi ni wadau wakubwa, tulitumia miaka miwili kwa
maandalizi, tuna hamu kubwa na matumaini ya kuona sasa Katiba Mpya
inapatikana.”
Rais Kikwete na Dk Shein
Jaji Warioba alisema Rais Kikwete ndiye
aliyeanzisha mchakato wa Katiba Mpya kwa nia njema na kwamba muda wote
amekuwa akifanya kazi ya kuusimamia mchakato huo pamoja na kazi za Tume
ya Mabadiliko ya Katiba akishirikiana kwa karibu na Dk Shein, hivyo bado
wana wajibu wa kuchukua hatua ili kukamilisha safari ya kupata Katiba.
“Sasa Bunge la Katiba lina matatizo, bado ni
wajibu wao (Rais Kikwete na Dk Shein), kuchukua hatua ili kupata Katiba
Mpya. Huu ni mchakato, awamu ya kwanza Bunge lilitunga sheria, ya pili
Tume ya Katiba ikafanya kazi, ya tatu Bunge Maalumu la Katiba na nne
wananchi watapiga kura. Mawazo yetu ni kusaidia mchakato huu ukamilike.
Tunataka ufanikiwe,” alisema akionya:
“Tusije tukajidanganya kama tusipofanikiwa
tutaendelea kwa usalama, kuna hatari ya amani ya nchi na usalama
kuvurugika.
Viongozi lazima waelewe hili kwani madai ya Katiba Mpya yalikuwapo zaidi ya miaka mitatu iliyopita. Wananchi wengi wanaamini kuna umuhimu wa kupata Katiba Mpya, tena wengi wa hali ya chini, ingawa viongozi ndiyo walioanzisha madai hayo.”
Viongozi lazima waelewe hili kwani madai ya Katiba Mpya yalikuwapo zaidi ya miaka mitatu iliyopita. Wananchi wengi wanaamini kuna umuhimu wa kupata Katiba Mpya, tena wengi wa hali ya chini, ingawa viongozi ndiyo walioanzisha madai hayo.”
Kauli hiyo ya Warioba imekuja huku maandalizi ya
kikao cha Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza tena vikao vyake Agosti
tano yakiendelea.
Aprili 16, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba aliiongoza Ukawa kutoka kwenye Bunge la Katiba akilalamikia CCM
kutowatendea haki kwa mambo mbalimbali ikiwamo kupinga mapendekezo yao
hata ya msingi, akisema hawawezi kuwa sehemu ya watu wanaosambaza chuki
na kuwa sehemu ya kuibomoa nchi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Siku chache baadaye, walianza kufanya mikutano nchi nzima kwa
kile walichodai kuwaeleza wananchi namna CCM inavyotaka kuchakachua
maoni yao yaliyokusanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Kwa upande wake, CCM imekuwa ikifanya mikutano
kuzunguka nchi nzima kueleza msimamo wake na sababu za wao kutaka
kuendelea kutumika kwa muundo wa Serikali mbili unaotumika sasa na
kubeza hoja za Ukawa.
Lakini jana Warioba alisema yeye na waliokuwa
wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya walifuatilia hali ilivyokuwa katika
Bunge Maalumu la Katiba na baada ya kuahirishwa... “Tukaamua tukutane
kwa siku tatu kama raia na kufanya tathmini kama raia, pia tuliamua
kukaribisha wasomi na baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba. Tuliwaalika
wasomi watano na wabunge wawili wa Bunge Maalumu la Katiba, Kingunge
Ngombale Mwiru na Profesa Abdul Sharif wa Zanzibar.
“Baada ya kuwasikiliza, tukafanya tafsiri yetu
wenyewe na kufikia mahali tukasema ni muhimu jukumu la Bunge Maalumu la
Katiba kuendelea. Liendelee kwa msingi wa kuimarisha mchakato wa Katiba
Mpya, walifahamu hili, wafikie makubaliano.
“Waangalie wapi wanatofautiana, wapi wanakwenda
sawa, waweke kando tofauti watoke na yanayowapatanisha ili kupata
matokeo ya kuwa na Katiba Mpya.”
Serikali mbili au tatu
Jaji Warioba alisema kipindi kilichopita Bunge
hilo lilishughulikia kanuni na kujikita zaidi katika mjadala wa muundo
wa Serikali mbili au tatu, mambo yaliyochukua muda zaidi, lakini mkutano
ujao utakuwa na mambo mengi zaidi.
“Muundo wa serikali mbili au tatu huo ulikuwa
ndiyo mjadala. Katika eneo hilo hata bunge lijalo kazi bado kubwa
inahitajika. Tunaweza kuzungumzia upungufu wa Serikali tatu, lakini bado
kuna umuhimu wa kuzungumzia udhaifu wa Serikali mbili:
“Bado matatizo ya Tanganyika kuvaa koti la
muungano, mgongano wa Katiba ya Zanzibar na Muungano, hatuwezi kunyamaza
tukaamini yataondoka. Pia lipo suala la maadili na miiko ya viongozi,”
alisema.
Warioba aliyefanya kazi katika Serikali tangu
Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, alitaja mambo mengine muhimu
kuangaliwa katika Bunge hilo kuwa ni utengano wa mihimili akisema lina
mtizamo tofauti, madaraka ya rais, ukomo wa uongozi na madaraka ya
wananchi kuweka au kuondoa mbunge madarakani, Tume huru ya uchaguzi,
Tume ya Haki za Binadamu na suala la mgombea binafsi.
Mwananchi
Mwananchi
0 comments:
Post a Comment