Kamati ya shindano la ulimbwende la Miss Tanzania, imesisitiza kuwa shindano hilo, litafanyika kama ilivyopangwa kufanyika Oktoba 11, katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. 

Awali kulikuwa na zuio la mahakama hivyo kutishia kutofanyika kwa shindano hilo.

Shindano la Miss Tanzania kwa mwaka huu litashirikisha warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali ya nchi ambao wanatarajiwa kuchuana Jumamosi ya wiki hii.

Hashimu Lundenga ni mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni waratibu wa shindano hilo, anasema kuwa mahakama imetupilia mbali zuio hilo.

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo anasema kuwa maandalizi yote yamekamilika.

Mratibu wa shindano hilo Vicky Kimaro anazungumzia ubora wa zawadi huku baadhi ya warembo wakisema wamejifua vilivyo kuelekea siku hiyo muhimu kwao.

Jumla ya warembo thelathini  wanatarajiwa kuchuana na mshindi ndiye atakayeweza kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya dunia.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top