TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Oktoba 8, 2014
Kocha wa timu ya Taifa ya Benin, Olle Didier
Nicolle ametaja kikosi cha wachezaji 18 kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars
itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mfaransa huyo ameita wachezaji 13 wanaocheza nje
ya nchi hiyo akiwemo kiungo Stephane Sessegnon wa West Bromwich Albion ya
Uingereza kwa ajili ya mechi hiyo ya Kalenda ya FIFA itakayoanza saa 11 jioni.
Wachezaji wengine katika kikosi hicho ni Didier
Sossa (AS Dragons FC de I’Oueme, Benin), Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive du
Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (FC Liefering, Austria), Sessi D’almeida (FC
Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed Aoudo (JS Saoura, Algeria) na Saturnin
Allagbe (US Krake, Benin).
Steve Mounie (HSC Montpellier, Ufaransa),
Farnolle Fabien (Clermont Foot Auvergne 63, Ufaransa), Jordan Adeoti (SM Caen,
Ufaransa), Michael Pote (Omonia Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis
Bordeaux, Ufaransa) na Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).
Jean Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Benin),
Nafiou Badarou (ASO Chlef, Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin),
Fortune Ore (US Krake, Benin) na Seibou Mama (US Krake, Benin).
Msafara wa timu hiyo utaanza kuingia nchini kesho
(Oktoba 9 mwaka huu) kwa nyakati tofauti, na utakuwa umekamilika (Oktoba 10
mwaka huu). Timu hiyo itafikia hoteli ya JB Belmont.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) leo (Oktoba 8 mwaka huu) linaadhimisha miaka 50 ya kujiunga na Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Katika kuadhimisha siku hii TFF ilipanga kufanya tafrija fupi ya kuwaenzi wale wote waliotoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania katika kipindi hicho cha miaka 50.
Hafla hii itafanyika katika siku
nyingine itakayopangwa.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment