Wanainchi wakiangalia Lori baada ya kuungua
Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii
Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii
Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa
Hii ni njia ya mlima sekenke
Moto ukimalizikia kwa mbaliii kama inavyoonekana
Lori
la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya Sekenke mkoani
Singida na kuua watu wanne hapohapo.
Chanzo cha ajali hiyo ni breki
kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo.Shuhuda
wa ajali hiyo Bwana Julius Chacha alipotoa taarifa amesema kwamba Lori
hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika
moto.
Akiendelea kuongea shuhuda huyo alisema walishindwa kutoa msaada
wowote kwa vile moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya
kuokolea.Watu wanne wamekufa papo hapo kutokana na ajali hiyo.Polisi
walikuwa bado hawajafika mpaka tunaondoka eneo la tukio.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment