Kiongozi wa jiji la Hong Kong C Y
Leung ametoa wito wa kusitishwa maandamano ambayo amesema yamedumaza
shughuli katika jiji zima.
Amesema kuwa maandamano hayo hayawezi kubadili msimamo wa China juu ya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.
Wakati huo huo Marekani imesema inafuatilia kwa karibu kinachoendelea Hong Kong na imeutaka utawala kuchukua hatua.
Katika
mkutano wa wanahabari msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema
Marekani inaunga mkono matakwa ya watu wa Hong Kong.
Makumi kwa mamia ya
waandamanaji wa Hong Kong wanaendelea na maandamano yao kwa siku
nyingine tena baada ya kudhoofisha maeneo muhimu ya jiji hilo wakati wa
mchana.
Wakati huo huo Marekani imesema inafuatilia kwa karibu kinachoendelea Hong Kong na imeutaka utawala kuchukua hatua.
Katika mkutano wa wanahabari
msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema Marekani inaunga mkono
matakwa ya watu wa Hong Kong.
"Duniani kote, na hii ni kweli
katika Hong Kong na maeneo mengine, Marekani inaunga mkono kimataifa,
uhuru, kama vile uhuru wa kukutana kwa amani na uhuru wa kujieleza.
Marekani inautaka utawala wa Hong Kong kuchukua hatua, na kwa upande wa waandamanaji kutoa maoni yao kwa amani"
BBC
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment