Rais Obama amekiri katika televishen
ya kitaifa kuwa Mashirika ya Marekani yalikosea katika kukadiria hatari
ya wapiganaji wa dola ya kiislam, Islamic State nchini Iraq na Syria.
Amesema
kuwa wapiganaji hao wenye uhusiano na Al Qaeda walitumia fursa ya
kutokuwepo serikali thabiti nchini Syria na kuongezewa nguvu zaidi na
vijana waliojiunga kupigania jihadi kutoka mataifa mengine.
Hata
hivyo Obama amesema wapiganaji hao waliwahi kuvurumishwa huko Iraq na
majeshi ya nchi yake yakishirikiana na kabila la Sunni.
Obama
amekiri vyombo vya Ujasusi vya Marekani zilikadiria vibaya uwezo wa
majeshi ya Iraq kupambana na wapiganaji wa kiislamu ambao wameteka
maeneo mengi nchini humo.
BBCSwahili
0 comments:
Post a Comment