Wahamiaji wa Kiafrika
Maafisa wa serikali nchini Yemen wamesema kuwa zaidi
ya wahamiaji arubaini wa Kiafrika wamezama baharini, baada ya mashua
walimokuwa wakisafiria kuzama, katika pwani ya kusini mwa nchi hiyo.
Manuwari ya jeshi la Yemen ambalo lilikuwa katika eneo hilo, imefanikiwa kuwaokoa wahamiaji wengine wapatao thelathini.
Wizara
ya ulinzi nchini Yemen imesema kuwa mashua hiyo iliyokuwa ikisafirisha
wahamiaji haramu, ilizama katika mkoa wa Kusini wa Shabwa, eneo ambako
maelfu ya wahamiaji wa Kiafrika huwasili kila mwaka.
Kwa mujibu wa shirika la Kimataifa la Uhamiaji
la IOM, wengi wa wakimbizi wanaojaribu kuvuka guba la Eden, wanatoka
Somalia na Ethiopia.
Shirika hilo limesema kuwa wahamiaji hao hufanya
safari ndefu na hatari ili kukwepa umasikini, unyanyazaji au vita
katika mataifa yao.
Baada ya kuwasili Yemen, wengi wao hutarajia
kupata kazi nchini Saudi Arabia na mataifa ya Guba, lakini mamia ya
wahamiaji wa Kiafrika hufa kila mwaka wakijaribu kuvuka eneo hilo la
Guba wakitafuta maisha bora katika mataifa ya ngambo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment