UTANGULIZI
Serikali inakusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne (K4) na cha Sita (K6) pamoja na Matumizi ya Alama Endelevu ya Mwanafunzi [Continuous Assessment (CA)]. Serikali imeamua kukusanya maoni haya kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika katika mitihani ya kuhitimu K4 na K6 havifanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari. Pia mfumo wa elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa. Kwa sasa kuna miundo mikuu miwili tofauti.

Muundo wa Kwanza ni upangaji wa viwango vilivyozoeleka ngazi ya Shule ambapo Alama Mgando (Fixed Grade Ranges) zifuatazo hutumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0 – 20.

Muundo wa Pili ni wa viwango vinavyotumiwa na Baraza la Mitihani la Taifa ambapo kuanzia mwaka 2012 Serikali iliamua kutumia mfumo wa Upangaji wa Alama Mgando (Fixed Grade Range) kwa K4 na K6. Katika mtihani wa K4 mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumo huu mpya ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. Kwa upande wa K6 Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E = 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39.

Vilevile, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi zitachangia asilimia hamsini (50%) na Mtihani wa wa mwisho utachangia asilimia hamsini (50%) pia. Hata hivyo, kumekuwa na mitizamo, maoni na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi. Mfumo huu hata hivyo hautumiki kwa wanafunzi wa kujitegemea (private candidates).

Serikali pia imedhamiria kufanya harmonization ya masuala ya alama katika mitihani ya K4 na K6 ili kupata muundo mmoja ambao utakuwa wazi kwa wadau wote wa elimu wa elimu ya sekondari. Lakini pia serikali imejikita katika kuhakikisha tathmini za wanafunzi katika ngazi mbalimbali zinakwenda sambamba na matarajio ya mitaala inayotumika.

Kwa kuwa wewe ni miongoni mwa wadau muhimu wa elimu, maoni yako yanahitajika sana ili tuweze kupata picha ya ujumla katika maeneo hayo mawili (upangaji wa viwango vya alama na matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi katika mitihani ya K4 na K6). Vilevile, maoni yako yatasaidia katika kutoa uamuzi wa kitaifa wa namna bora zaidi ya upangaji viwango vya alama kwa ajili ya Wahitimu wa K4 na K6 utakaoanza kutumika sasa na miaka ijayo. Kwa hiyo, tunaomba ujibu maswali UTANGULIZI

Serikali inakusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne (K4) na cha Sita (K6) pamoja na Matumizi ya Alama Endelevu ya Mwanafunzi [Continuous Assessment (CA)]. Serikali imeamua kukusanya maoni haya kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika katika mitihani ya kuhitimu K4 na K6 havifanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari. Pia mfumo wa elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa. Kwa sasa kuna miundo mikuu miwili tofauti.

Muundo wa Kwanza ni upangaji wa viwango vilivyozoeleka ngazi ya Shule ambapo Alama Mgando (Fixed Grade Ranges) zifuatazo hutumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0 – 20.

Muundo wa Pili ni wa viwango vinavyotumiwa na Baraza la Mitihani la Taifa ambapo kuanzia mwaka 2012 Serikali iliamua kutumia mfumo wa Upangaji wa Alama Mgando (Fixed Grade Range) kwa K4 na K6. Katika mtihani wa K4 mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumo huu mpya ambapo: A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49, F = 0 – 34. Kwa upande wa K6 Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E = 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39.

Vilevile, Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 imeelekeza kwamba katika kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi wa elimu ya sekondari, Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi zitachangia asilimia hamsini (50%) na Mtihani wa wa mwisho utachangia asilimia hamsini (50%) pia. Hata hivyo, kumekuwa na mitizamo, maoni na mapendekezo tofauti katika muundo na matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi. Mfumo huu hata hivyo hautumiki kwa wanafunzi wa kujitegemea (private candidates).

Serikali pia imedhamiria kufanya harmonization ya masuala ya alama katika mitihani ya K4 na K6 ili kupata muundo mmoja ambao utakuwa wazi kwa wadau wote wa elimu wa elimu ya sekondari. Lakini pia serikali imejikita katika kuhakikisha tathmini za wanafunzi katika ngazi mbalimbali zinakwenda sambamba na matarajio ya mitaala inayotumika.

Kwa kuwa wewe ni miongoni mwa wadau muhimu wa elimu, maoni yako yanahitajika sana ili tuweze kupata picha ya ujumla katika maeneo hayo mawili (upangaji wa viwango vya alama na matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi katika mitihani ya K4 na K6). Vilevile, maoni yako yatasaidia katika kutoa uamuzi wa kitaifa wa namna bora zaidi ya upangaji viwango vya alama kwa ajili ya Wahitimu wa K4 na K6 utakaoanza kutumika sasa na miaka ijayo. Kwa hiyo, tunaomba ujibu maswali yafuatayo yaliyoko katika dodoso, Jaza na Utume katika Barua pepe hii: moet@moe.go.tz
 icon Bofya hapa kupata dodoso
Chanzo: Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

Top