RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekwenda Mozambique leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambako atahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Mkutano huo uliopangwa kufanyika baadaye leo, utakuwa chini ya uenyekiti wa Rais Emilio Armando Guebuza, Rais wa Mozambique ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa SADC.


Kikao hicho kitajadili maendeleo katika juhudi za SADC kutafuta ufumbuzi wa migogoro ambayo Jumuia hiyo imekuwa inaishughulikia karibuni na inayohusu nchi wanachama wa Jumuia hiyo – yaani hali ya kisiasa katika Madagascar na Zimbabwe na hali ya kiusalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako majeshi ya waasi wa M23 yanakabiliana na majeshi ya Serikali ya Rais Joseph Kabila.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top