Kituo cha sheria na haki za binadam (LHRC) kimezindua ripoti ya kumi na moja ya mwaka 2012 ya uchunguzi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu na changamoto zilizojitokeza.

Ripoti hiyo imebainisha tathmini katika mambo mbalimbali likiwemo suala la  uhuru wa vyombo vya habari hapa nchini, kupinga unyanyasaji wanaofanyiwa baadhi ya wamiliki wa vyombo vya habari, kuandika habari kwa maslahi binafsi au jamii, kuteswa, kutishiwa maisha na kuuwawa kwa aliyekuwa mwandishi wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud Mwangosi .

Katika tukio la kuuwawa kwa Daud Mwangosi ripoti hiyo imefanya tathmini na kubaini kuwa, uhusiano baina ya ya polisi na waandishi wa habari mkoani Iringa si wa kuridhisha, na kueleza matukio kadhaa ya kunyanyaswa kwa  waandishi wa habari .

Mambo mengine yaliyobainishwa ni pamoja na elimu, afya na haki ya kuishi ambapo kwa mujibu wa ripoti ya haki za binadamu kwa mwaka 2012 , jumla ya watu 31 wameuawa na vyombo vya dola huku taarifa hiyo pia ikionyesha bado wananchi wanachukua sheria mkononi katika utatuzi wa migogoro kadhaa.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top