Waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Mhongo.
 
Serikali imeingia makubaliano na kampuni ya General Electric ya Marekani  kwa ajili ya uzalishaji wa wa umeme wa megawati 400 ambao utaweza kupunguza adha ya upatikanaji wa nishati hiyo hapa nchini.
 
Akizungumza katika hafla fupi ya kutia saini  makubaliano, Waziri wa nishati na madini Profesa Sospeter Mhongo amesema kupitia  kampuni ya Symbion watashirikiana katika mradi huo ambao amesema utaleta tija kwa taifa.
 
Profesa Mhongo amesema kuwa mradi ukizalisha umeme wa ziada unaweza kuliongezea pato taifa kwani utaweza kuuzwa katika nchi jirani ambazo zina mahitaji ya nishati hiyo.
 
Waziri huyo amesema kuwa uwekezaji  huo ni moja ya mikakati ya serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme wa uhakika na kuchochea jitihaza za kujileta maendeleo.
 
Mradi huo unataraji kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itaanza kutekelezwa hapo mwakani mara baada ya upembuzi yakinifu kukamilika.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top