JESHI la polisi mkoani
Katavi limewaasa wananchi kujihadhari na wageni wasioeleweka shughuli
zao na mahali wanakotoka kutokana na kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu
vinavyodaiwa kufanywa na wageni kwa kushirikiana na baadhi ya wakazi wa mkoa
huo.
Hayo aliyasema katika mkutano
wa hadhara wa polisi jamii kwenye makazi ya wakimbizi ya Katumba wilaya ya
Mlele ambapo Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi, Dhahir Kidavashari, alisema kuwa katika
kipindi cha kiangazi kumekuwa na wimbi la wahalifu kuongezeka katika mkoa wake
kutokana na mwingiliano mkubwa wa wananchi na wafanyabiashara wa ndani na nje ya mkoa huo.
Alisema katika matukio ya
hivi karibuni vitendo vya uporaji, unyang’anyi
wa kutumia silaha na hata mauaji vimekuwa vikiendelea kutokea ingawa polisi imefanikiwa kuwakamata wahalifu kwa kuwa kuna baadhi ya wageni wanashirikiana katika uhalifu na baadhi ya wakazi wa mkoa huo wasio waaminifu.
Alitolea mfano katika tukio la
hivi karibuni ambapo baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Ilebula B’ kata ya Katuma
wilaya ya Mpanda walivamiwa na majambazi waliokuwa na silaha aina ya SMG na
kupora fedha na simu zao majira ya saa
sita usiku katika tukio la Agosti 2, 2013.
Aliwataja walioporwa katika
tukio hilo ambalo awali majambazi walifyatua risasi mbili hewani ni ndugu Juma
Kubu (38) aliporwa fedha taslimu shilingi 132,000/= na simu aina ya Techno
yenye thamani ya shilingi 40,000/=, ndugu Moshi Masanilo (23) aliporwa baiskeli
moja aina ya Phoenix yenye thamani ya shilingi 150,000/=, Thelethini Msoke (45)
aliporwa bia sita na soda nne vyote vikiwa na thamani ya shilingi 16,000/=.
Wengine walioporwa
aliwataja kuwa ni Alphonce Charles (23) aliporwa fedha taslimu shilingi
130,000.= na simu aina ya Yxtel yenye thamani ya shilingi 65,000/=, Jumanne
Kashindye (28) aliporwa simu aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi 40,000/=,
Christina John (42) aliporwa fedha taslimu shilingi 120,000/= na simu aina ya
Techno yenye thamani ya shilingi 45,000/= na ndugu Sisilia Ezekiel (49)
aliyeporwa simu aina ya Oking yenye thamani ya shilingi 60,000/=.
Aidha Kamanda wa polisi
mkoani hapa aliwataja wengine waliioporwa kuwa ni Regina Ezekiel (37) ambaye
aliporwa fedha taslimu shilingi 6,000/= na simu aina ya Nokia yenye thamani ya
shilingi 40,000/=, ndugu Cosmas Mathia (42) aliyeporwa shiligi 70,000/= na simu
aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi 40,000/=, Ndilanha Charles (40)
aliyeporwa simu aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi 30,000/= na ndugu Dotto
Peter (29) aliyeporwa simu aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi 35,000/=.
Alisema katika tukio hilo
ni dhahiri kuwa majambazi yalifikia katika hatua mbaya kwani walivamia kitongoji
kizima ingawa hawakujeruhi mtu yeyote lakini bado ipo haja kwa jeshi la polisi
na wananchi kuchukua hatua za makusudi ili kuutokomeza kabisa uhalifu wowote mkoani Katavi.
Pamoja na kuwashukuru
wananchi waliotoa ushirikiano uliopelekea kukamatwa kwa watuhumiwa wa uvamizi
huo wapatao wanne wanaodaiwa kushiriki katika kuvamia kitongoji na kuwapora
wananchi ambapo kamanda aliwataja waliokamatwa kufuatia tukio hilo kuwa ni
ndugu Sengwa Mojo (43) , ndugu Amosi Ngasa (43), Barabashi Kasomi (43) na ndugu
Mojo Nsengwa (43) wote kabila lao ni Wasukuma wakazi wa kitongoji cha Ilebula
wilaya ya Mpanda.
Alisema watuhumiwa hao
walikamatwa kufuatia taarifa za baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho
ziliziopelekea kupata baadhi ya simu zilizoporwa majumbani kwao baada ya
kupekuliwa na askari polisi ambapo upelelezi unaendelea na watuhumiwa hao
watafikishwa mahakani ingawa maelezo yanaonesha kulikuwa na mpango wa muda
mrefu wa kutaka kuvamia kitongoji hicho kwa kutumia silaha lakini wananchi hao
hawakuona umuhimu wa kutoa taarifa polisi hadi walipovamiwa.
Aliwataka wananchi mkoani
humo kuwa makini na nyendo za baadhi ya wananchi wenzao wanaotafuta utajiri kwa
njia zisizo halali na kutoa taarifa mapema ili kuweza kuzuia tukio badala ya
kuwa maarufu wa kutoa taarifa za uhalifu baada ya kutokea kwani dhana ya jeshi
la polisi ni kuzuia uhalifu kabla ya kutokea
Afa kwa kunywa gongo
Katika tukio lingine imeripotiwa kuwa ndugu
Aloyce Alfredy
Sali, ( 32) alikutwa akiwa amefariki dunia chumbani kwake kwenye
nyumba aliyokua amepanga baada ya kunywa pombe aina ya gongo.
Taarifa zilizopatikana mjini Mpanda
zinadai kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 3, 2013 majira ya saa kumi na moja
jioni ambapo marehemu alikwenda katika eneo maarufu kwa kuuza pombe haramu ya moshi
maarufu kama pombe ya gongo liitwalo Mpandahoteli katika baa ya MWANDOSYA ambako alikunywa pombe hiyo ya gongo.
Ilielezwa kuwa baadaye marehemu alilejea
nyumbani kwake anakoishi peke yake bila familia na kuingia ndani na kulala hadi
kesho yake tarehe Agosti 4, 2013 majira ya saa sita mchana ambapo inadaiwa kuwa Marehemu hakuonekana hadi hali iliyosababisha majirani kuingiwa na wasiwasi na kuamua kufatilia kwa karibu ambapo walibaini ndugu Aloyce alikuwa ameshafariki jambo lililowafanya kutoa taarifa kituo cha Polisi Mpanda.
Kamanda wa polisi mkoani Katavi,
Dhahiri akizungumza na gazeti hili alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na
kueleza kuwa Uchunguzi wa tukio hilo unaonesha chanzo cha kifo cha marehemu ni
kutokana matumizi ya pombe ya moshi aina ya gongo yaliyokithili pasipo kula
chakula.
Ajali yaua na kujeruhi
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Akizungumzia
matukio mengine kamanda wa polisi Kidavashari alisema kuwa Agosti 3, 2013 majira
ya saa mbili usiku katika kijiji cha Ikaka kwenye barabara ya Mpanda
kwenda Karema gari yenye namba za usajiri T707AFQ aina ya Canter inayomilikiwa
na Bwanali Kondowe mkazi wa Makanyagio
mjini Mpanda lilipinduka na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye haijafahamika.
Alisema katika tukio hilo watu watano walijeruhiwa
na kupelekwa hospitali kuu ya Mpanda na kwa matibabu na baadaye waliruhusiwa
kutoka hospitali kutokana hali yao kuwa njema ambapo aliwataja majeruhi kuwa ni
Cletus Isack(21), Erick Itala (21), Juma Yasini (20), Digas Elisha (25) na Musa Elisha (20) wpte wakazi wa wilaya ya
Mpanda mkoani Katavi.
Aidha kamanda Kidavashari alisema chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva
ambaye bado anaendelea kutafutwa.
Chanzo: Sumiablog
0 comments:
Post a Comment