![]() |
| Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi Bwana James Mbatia |
Wakati
makundi mbalimbali yanatoa maoni ya katiba mpya,chama cha NCCR Mageuzi
kimependekeza kuwa Lugha ya Kiswahili inatakiwa kutumika katika sekta muhimu
zote za mawasiliano.
Mwenyekiti
wa chama cha NCCR Mageuzi bwana James Mbatia alisema lugha ya Kiswahili
inatakiwa kuthaminiwa na kuandikwa katika katiba mpya,sheria za nchi ziandikwe
kwa kiingereza na mahakama kuu ziitumie kama lugha ya mawasiliano katika
utendaji wake.
Mwenyekiti
huyo aliwataka watanzania kuachana na kasumba na mtazamo potofu wa kupenda
kujifunza na kuona lugha za kigeni ndiyo bora na kudharau Kiswahili ambayo
ndiyo sehemu ya utamaduni wao.
Bwana
Mbatia alisema inashangaza kuona Wataalam kutoka Kenya wakipata fursa
mbalimbali za ajira kupitia lugha ya Kiswahili wakati Watanzania wakishindwa
kuzipata licha ya kujivunia kuwa ni lugha ya Taifa.
Imeelezwa
kuwa nchi nyingi zilizopiga hatua kimaendeleo zimekuwa zikitumia lugha za asili
katika mawasiliano hivyo jitihada za makusudi zinahitajika kukiendeleza zaidi
Kiswahili.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment