Mratibu wa mtandao wa katiba initiative akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwasilisha maoni ya Jamii za   wafugaji

Baadhi ya wawakilishi wa mtandao wa Katiba initiative unaopigania haki za wafugaji wakiwa nje ya jengo la Tume ya Mabadiliko ya katiba mara baada ya kuwasilisha mapendekezo yao.

 Jumuiya ya wafugaji imetoa mapendekezo ya kutaka masuala ya  ardhi na rasilimali za nchi yanatakiwa  kuwekwa  katika katiba mpya ijayo ili kuepusha migongano inayojitokeza mara kwa mara katika jamii.

 Mratibu wa  Mtandao wa katiba initiative WILLIAM OLE NASHA amesema  rasilimali ardhi,mali asili na rasilimali watu zinatakiwa kutumika  ipasavyo kwa mustakabali wa maendeleo ya wananchi wote badala ya kuwanufaisha watu wachache.



Mratibu huyo amesema miongoni mwa vitu wanavyotaka ni kuhakikisha kuwa mgawanya na matumizi  ardhi unawekwa kikatiba na kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima pamoja na



Mratibu huyo amesema wafugaji wamekuwa wakitoa mchango mkubwa wa maendeleo tangu taifa la Tanzania kujipatia uhuru lakini kila wakati wamejikuta wakinyanyaswa kwa kuhamishwa kila wanapoweka makazi.



Baadhi ya wawakilishi wa makundi ya wafugaji wamesema wanataka kuona rasilimali kama rasilimali asili kama misitu,madini na mbuga za wanyama zinawafaidisha pia wenyeji wanaoishi kuyazunguka maeneo ya yenye vivutio vya utalii.
 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top