Serikali
imesema inafanyia marekebisho sheria kandamizi ili kuleta usawa katika
jamii ili kupata mwelekeo wa pamoja katika masuala ya jinsia.
Akifungua
semina ya maboresho ya sekta ya sheria kwa watumishi wa idara mbalimbali
za sheria,Waziri wa katiba na Sheria Mathias Chikawe amesema kuwa kuna umuhimu
wa sheria ambazo hazifai kwa sasa zifanyiwe marekebisho kwa ustawi wa jinsia
zote katika jamii.
Naye
Mshauri wa Wanyinda Phillip Katto amesema kuwa suala la usawa wa kijinsia
katika jamii ni suala la mchakato wa muda mrefu kutokana tamaduni mila na
desturi zilizopitwa na wakati ambazo zilimfanya mwanamke kushindwa kumiliki
ardhi.
0 comments:
Post a Comment