Deodatus Balile Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jamhuri na  mmoja wa wawakilishi wa Jukwaa la wahariri akiongea na waandishi wa habari kuhusu mapendekezo ya jukwaa hilo yeye aliwasilisha uhuru wa vyombo vya habari,haki ya kutoa mawazo na haki ya kupata habari.

Jukwaa la wahariri  limetoa mapendekezo kuwa suala la uhuru wa vyombo vya habari ni suala la msingi ambalo linatakiwa kupewa kipaumbele katika katiba mpya kwa ustawi wa tasnia ya habari.

Mhariri Mtendaji wa gazeti la Jamhuri ,ambaye ni Mmoja wa wakilishi wa Jukwaa hilo Deodatus Balile amesema uhuru wa vyombo vya habari utaifanya tasnia ya habari kutokandamizwa wala kutoshitakiwa kwa kesi ambazo hazina mantiki.

Bwana Balile amesema sheria nyingine ambayo kimsingi ni muhimu kwa jamii ni kuhusiana na haki ya kujieleza na kupata habari pasipo vikwazo vyovyote ili kumuwezesha mtu yeyote kupata ama kutoa habari kwa mujibu wa katiba.
Wakati vyombo vya habari vikizidi kuongezeka kila uchao,bado kuna sheria ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kila uchao kudaiwa kuminya uhuru wa vyombo hivyo ikiwemo sheria ya magazeti ya mwaka 19 TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top