BARCELONA NA BAYERN MUNICH VITANI LEO
ULAYA
Barca wakitoka vichwa chini
Barca wakiwa mazoezini
Waswahili wana
msemo wao usemao “Mwenzako akinyolewa zako tia maji”, Madrid safari yao
imefikia tamati Jumanne usiku huku
wakiathiriwa na matokeo ya mchezo wa kwanza, watani zao wa jadi, FC Barcelona
nao leo wanapambana na miamba ya Ujerumani FC Bayern Munich katika dimba la
Camp Nou huku Barca wakiwa na kumbukumbu ya kutandikwa mabao 4-0 Allianz
Arena huko jijini Munich.
FCBarcelona wanahitaji magoli 5 – 0. Na endapo
watashinda magoli 4 – 0 mechi itaongezwa
dakika 30 kama mshindi wa jumla hatapatikana changamoto ya mikwaju ya penati
itaamua timu itakayosonga hatua ya fainali itakayopigwa katika dimba la Wembley
huko jijini London Uingereza.
Mshindi wa jumla wa mechi hiyo nusu fainali baina ya FC Barcelona na Bayern Munich
atakutana na Borussia Dortmund timu ambayo imekata tiketi kwa kuwafurusha
mabingwa wa mara TISA wa michuano ya ligi ya Mabingwa Ulaya Real Madrid.
REAL MADRID YATUPWA NJE ULAYA, LICHA YA
USHINDI WA 2 – 0
Karim Benzema akifunga bao
Sergio Ramos akishangilia bao alilofunga
Kocha Jose Mourinho akipagawa wakati wa mechi
Borussia
Dortmund wakishangilia ushindi
Licha ya Real
Madrid ya Hispania kuibuka na ushindi wa magoli 2 – 0 dhidi ya Borussia
Dortmund ya Ujerumani timu hiyo imetupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa
barani Ulaya katika mechi iliyochezwa katika dimba la Santiago Bernabeu jijini
Madrid.
Matokeo hayo
yameitupa nje Real Madrid kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza nchini
ujerumani ambapo Mourinho alipiga kipigo cha mbwa mwizi cha mabao 4-1 na baada
ya kushinda JANA kwa mabao mawili Madrid wanatoka kwa wastani wa mabao 4-3.
Miamba hiyo ya
Hispania ilikuwa inahitaji kufunga magoli 3 – 0 ili iweze kutinga fainali walau
kwa faida ya goli la ugenini lakini magoli hayakuweza kuwatoa kimasomaso
Mshindi wa mechi baina ya FC Barcelona na Bayern
Munich atakutana na Borussia Dortmund timu ambayo imekata tiketi kwa
kuwafurusha mabingwa wa mara TISA wa michuano ya ligi ya Mabingwa Ulaya Real
Madrid.
Ilikuwa mechi ngumu kwa vijana wa Mourinho kwani walilazimika
kumaliza kipindi cha kwanza wakiwa 0-0 na kipindi cha pili kilipoanza bado
mambo yalikuwa magumu mpaka dakika ya 83 ambapo waliandika bao la kwanza
kupitia kwa Mfaransa Karim Benzema akipokea pasi nzuri kutoka kwa Mjerumani
Mesut Ozil.
Na katika dakika
ya 88 beki machachari Sergio Ramos alimalizia pasi maridhawa ya Karim Benzema
na kuzamisha gozi kambani, hata hivyo matokeo hayo hayakufua dafu kufuatia kipigo
cha 4-1 ugenini.
Katika kipindi
cha kwanza cha mchezo huo Real Madrid walicheza vizuri zaidi ya wapinzani wao
lakini walishindwa kupangua ngome imara ya Kocha Flopp aliyetamba toka awali
kuwa hawataweza kuwafunga, lakini kipindi cha pili waliachia na kufungwa, kama
Madrid wangekuwa makini wangewatoa baada
ya kupoteza nafasi muhimu.
Ozil hatasaulika
kwa mashabiki wa soka wa Real Madrid baada ya kupoteza nafasi muhimu za kufunga
mabao ambayo yangewapeleka dimba la taifa la Wembley nchini Uingereza kucheza mchezo
wa fainali.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI






0 comments:
Post a Comment