Kikosi cha Zima moto
na uokoaji cha Halmashauri ya mji wa Njombe kwa kushirikiana na wananchi
wakitoa mwili wa Mhandisi wa Maji katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Abdalah
Mgambo aliyefariki baada ya kutumbukia kwenye kisima jana katika Uwanja wa ukumbi wa
Turbo Mjini Njombe.
Mwili wa Eng. Abdalah
Mgambo ukionekana kwa mbali kwenye gari la Polisi wakati wa kuupeleka katika hospitali ya Kibena
kwa ajili ya kuuhifadhi.
Wa pili kushoto ni
Mhandisi wa Maji Halamshauri ya Mji wa Njombe Eng. Abdalah Mgambo enzi za uhai
wake wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Kilele cha Wiki ya Maji March 22 mwaka huu katika kijiji cha
Igominyi.
Marehemu Abdalah Mgambo enzi za Uhai wake akisoma taarifa ya
Hali ya maji katika halmashauri ya Mji wa Njombe mwezi machi 22 mwaka huu
wakati wa kilele cha wiki ya Maji Igominyi Njombe.
.............................................................
Taarifa toka eneo la Tukio zinasema kuwa marehemu Abdalah
Mgambo alikuwa katika Baa yake eneo la Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe kisha
akamuaga mke wake kwamba anatoka nje kujipumzisha kwenye gari lake majira ya
saa moja jioni jana April 30.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida akatoweka ghafla na kisha kadi yake ya Benki ya NMB Ilikutwa nje ya Kisima cha Maji kilichopo katika uwanja wa Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida akatoweka ghafla na kisha kadi yake ya Benki ya NMB Ilikutwa nje ya Kisima cha Maji kilichopo katika uwanja wa Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe.
Akizungumza na Mtandao huu wa www.gabrielkilamlya. blogspot.com
eneo la Tukio mara baada ya kuuokoa mwili wa Mhandisi huyo, Afisa mtendaji wa
Kata ya Njombe Mjini Bwana Donald Mng'ong'o amesema kuwa leo asubuhi amepata
taarifa toka kwa mke wa marehemu kuwa mme wake alitoweka ghafla na mara baada ya kuikuta
kadi ya ATM nje ya kisima cha maji ndipo wakachukua jitihada za kuanza kutafuta
kwenye kisima hicho kwa kushirikiana na kikosi cha Zima moto na Uokoaji cha
Halmashauri ya Mji wa Njombe.
Bwana Mng'ong'o amesema kuwa mwili wa marehemu Abdalah Mgambo umepatikana leo mnamo majira ya saa tisa jioni na kupelekwa katika Hospitali ya Kibena kwa ajili ya kuhifadhiwa.
0 comments:
Post a Comment