Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (PPFT), Askofu Pius Ikongo 
SIKU moja baada ya Ikulu kuliumbua Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania (PCT) kwamba hawakuwasilisha majina ya uteuzi kwa Rais Jakaya Kikwete, wameanza kushikana uchawi kumsaka aliyesababisha majina hayo kutofika Ikulu.
 
Hayo yamethibitishwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Ushirika wa Wachungaji wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (PPFT), Askofu Pius Ikongo, alipokuwa akizungumza na  Tanzania Daima.

Akizungumzia kuhusu tamko hilo la Ikulu, Askofu Ikongo alisema kuwa wanafanya uchunguzi kumnasa aliyesababisha kutofika majina hayo mezani kwa Rais Kikwete.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top