Shirikisho la kimataifa la msalaba
mwekundu, limesema kuwa kikundi kingine cha wahudumu wa afya
kilishambuliwa Jumanne Kusini Mashariki mwa Guinea walipokuwa
wakikusanya miili ya watu waliofariki kutokana na Ebola.
Mfanyakazi mmoja wa shirika hilo, anauguza majeraha baada ya kujeruhiwa vibaya katika shambulizi hilo katika eneo la Forecariah.
Kwa mujibuwa maelezo ya mkazi mmoja, jamaa wa wagonjwa waliofariki walianza kuwashambulia
wafanyakazi hao sita wa kujitolea,
kuwashambulia kwa mawe na kisha kuharibu magari yao.
Huu ni uvamizi wa hivi karibuni dhidi ya wahudumu wa afya ambao bila shaka unakwamisha juhudi za kupambana na ugonjwa huo mkali.
Wiki jana madaktari wengine na wandishi wa habari walishambuliwa Magharibi mwa nchi hiyo.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment