Mwuguzi mmoja nchini Kenya amehukumiwa kifo baada ya mwanamke aliyemsaidia kuavya mimbia kufariki miaka mitano iliyopita.
Nchini
Kenya kuavya mimba ni kinyume cha sheria ingawa matabibu kadhaa
huendesha shughuli hizo kisiri kwa sababu mapato yake ni makubwa.
Jackson
Namunya Tali, mwenye umri wa miaka 41, amehukumiwa kifo na Jaji
Nicholas Ombija mjini Nairobi, baada ya kupatikana na kosa la
kusababisha kifo cha msichana Christine Atieno katika kituo cha afya
anachosimamia .
Kwa mujibu wa taarifa ya mashahidi, Msichana Atieno
alitunga mimba ambayo hakutarajia na mnamo Julai, mwaka 2009, na
kuamua kutafuta msaada kwa Tali katika kituo chake cha afya katika eneo
la Gachie, viungani mwa jiji la Nairobi ambapo alitaka kuavya mimba hiyo.
Jaji
aliambiwa Kwamba licha ya jaribio la kuitoa mimba hiyo haikutoka na
badala yake mtoto aliyekua tumboni alikufa, hali iliyosababisha marehemu
kuvuja damu nyingi.
Mshtakiwa alipogundua hali ilikua mbaya alianza kumpa msichana huyo madawa ya maumivu kisha akampeleka katika hospitali ndogo ya Kaunti ya Kiambu.
Wahudumu wa afya katika
hospitali ya Kiambu walipendekeza mgonjwa kupelekwa kwa matibabu maaluum
katika hospitali ya nyingine ambapo angepokea matibabu ya dharura kwani
hali yake ilikuwa mbaya.
Hata hivyo msichana huyo, ambaye wakati
huu wote alikuwa akivuja damu akiwa ndani ya gari la mshtakiwa alifariki
dunia hivyo muuguzi aliyemhudumia kulaumiwa kwa kifo hicho na kisha kushtakiwa.
Hii ndio hukumu kali zaidi kutolewa nchini Kenya kuhusiana na kifo kutokana na kuavya mimba.
Nchini Kenya kutoa haikubaliwi ila ikiwa maisha ya mama yako hatarini
Mjadala
ya kuhalalisha uavyaji mimba umevutia hisia kali nchini Kenya wanaounga
wakisema itasaidia afya ya uzazi huku wapinzani wakisema ni mauaji ya
kiumbe asiye na hatia.
BBCSwahili
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment