
SAKATA la nyongeza ya posho limechukua sura mpya baada ya Mwenyekiti
wa muda wa Bunge Maalumu la Katiba, Pandu Ameir Kificho, kuunda kamati
ya watu sita kulishughulikia.
Kificho alisema kamati hiyo italishughulikia jambo hilo na kuishauri
serikali namna bora ya kulifanya ili wajumbe waifanye kazi kwa ufanisi
zaidi.
Juzi wajumbe wa Bunge hilo walikuwa wakipinga kiwango cha posho ya
sh 300,000 wanazopewa kwa siku, wakitaka walipwe sh 500,000 au sh
700,000 kwa madai kuwa gharama za maisha mjini Dodoma zimepanda.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment