Mji wa Johannesburg umemiminika watu waliojitokeza kumkumbuka Mandela na kutoa rambi rambi zao kwa jamii, familia na marafiki wao.

Viongozi duniani pia wameendelea kutuma rambirambi zao kufuatia kifo cha Mandela.

Kifo cha Mandela kilitangazwa hapo jana Alhamisi saa za usiku na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma aliyesema kuwa Afrika Kusini inaomboleza kumpoteza kiongozi huyo waliyemuenzi sana kama mtoto wao, baba yao na kiongozi wa taifa hilo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top