MSEMAJI wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Glory Mziray
hivi karibuni alisema Mkoa wa Njombe, Mbeya na Iringa ni vinara
wanaoongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini.
Alisema Njombe inaongoza kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa
asilimia 9.1 na Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya tatu kwa asilimia 9.
Mikoa mingine na asilimia za maambukizi katika mabano ni Ruvuma (7.2),
Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani
(5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).
Mikoa mingine aliyoitaja ni Mara (4.5), Mwanza (4.2), Mtwara (4.1),
Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8), Singida
(3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja
(1.9) na Pemba (0.3).
Mziray alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka
juzi hadi mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo, alisema maambukizi ya
Ukimwi yamepungua kwa kasi ndogo.
Alisema Watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu
Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi wanafikia asilimia 60 jambo
linalosababisha kuwepo mwamko mdogo wa kubadili tabia.
Kuhusu tohara kwa wanaume, alisema inapunguza maambukizi ya Ukimwi
kwa asilimia 60 na kusisitiza kuwa ipo haja ya kutoa elimu zaidi juu ya
uelewa wa ugonjwa huo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment