Na Gervas Mwatebela na mashirika
Wakati Desemba 9 mwaka 2012 ilikuwa siku ya furaha kwa Tanzania bara ikisherehekea miaka 51 ya Uhuru tangu kujikomboa kutoka katika minyororo ya wakoloni wa Uingereza mwaka 1961,nyota wa Barcelona na Argentina Lionel Messi alikuwa akifurahia mafanikio mengine katika soka.

Ilikuwa siku muhimu kwa Lionel Messi kwa sababu aliweza kuvunja rekodi ya nguli wa soka wa Ujerumani ambaye ulimwengu uliwahi kumshuhudia,huyu si mwingine bali ni Gerd Muller akiichezea Bayern Munich ya Ujerumani alifunga magoli 85 kwa mwaka mmoja (1972). 

Gerd Muller
Lakini pia watu wanatakiwa kufahamu kuwa Gerd Muller (67) alikuwa shujaa wa muda wote wa Ujerumani akifunga magoli 68 katika mechi za kimataifa  62 huku akifunga magoli 365 katika mechi 427 katika ligi kuu ya Bundesliga huko Ujerumani.
Messi alivunja rekodi hiyo wakati Barcelona ikicheza na Real Betis na kufunga goli la 85 na 86 hivyo kumfanya mchezaji aliyevunja rekodi ya magoli 85 ya Muller.
Hata hivyo rekodi hiyo ya Lionel Messi na Gerd Muller inaonekana kupingwa na chama cha soka nchini Zambia FAZ ambacho kimedai Godfrey Chitalu (kwa sasa marehemu) aliwahi kufunga magoli 107 katika mwaka mmoja yaani kuanzia februari hadi Desemba 1972.Hata hivyo shirikisho la kandanda ulimwenguni FIFA linaonekana kutokuwa na kumbukumbu hizo.

Godfrey Chitalu

Chitalu alizaliwa Oktoba 22,1947 Luanshya,Rhodesia ya Kaskazini (kwa sasa Zambia) ikiwa chini ukoloni wa Uingereza,nguli huyo wa Zambia alifariki April 27 mwaka 1993 akiwa na timu ya taifa ya Zambia iliyopata ajali ya ndege pwani ya Gabon na kuua wachezaji na maafisa wote waliokuwamo.
Chitalu aliwahi kupata tuzo ya mwanaosoka bora wa Zambia mara tano amechezea timu nyingi ikiwemo Kitwe United na Kabwe Warriors kwa mafanikio makubwa.
Baadhi wachambuzi wa soka wameoneshwa kushangazwa na chama cha soka nchini Zambia FAZ kushindwa kusema chochote kwa ajili ya kuweka takwimu sawa tangu mwaka 1972 mpaka sasa ambapo inaonesha hiyo ingekuwa rekodi ya miaka 40.
Rais Mstafu Keneth Kaunda
Mtafiti wa mambo ya soka Jerry Muchemba kutoka Zambia alisema kinachotofautisha nchi iliyoendelea kisoka na nchi za Kiafrika ni namna uwekaji wa kumbukumbu sahihi unavyotiliwa mkazo ili kutambuliwa kama rekodi sahihi.
’Rekodi rasmi zinapatika kwa chama cha soka chenye mikakati na mipangilio thabiti ambayo itaonesha timu ya taifa imefunga magoli mangapi,wachezaji wamecheza mechi ngapi na wamefunga magoli hayo kwa mechi za aina gani kirafiki au kimashindano’’,alisema Muchemba.
Muchemba anasema kwa bahati mbaya hakuna rekodi za muhimu kama hizo zikitolewa na shirikisho la kandanda Zambia-FAZ ili watu waweze kujua hivyo kila mtu anabashiri tu kwa utashi wake.

Ukiangalia kiundani kuna vitu vitatu elimu kujua umuhimu wa kutunza kumbukumbu,kuzitangaza kwenye mitandao rekodi mbalimbali za wachezaji katika mitandao ili iwe rahisi kwa wadau kuzijua kwa urahisi.
Muchemba anasema kwa kiasi kikubwa ameweza kuisadia FAZ kupata rekodi mbalimbali kupitia machapisho na mtandao wake.
Je ni aibu iliyoje kwa chama kushindwa na kuwa na kumbukumbu muhimu za wachezaji na timu za taifa  halafu  mtu baki ndiye awe nazo? Tafakari....
Wakati FAZ ikidai Chitalu ndiye aliyevunja rekodi ya Gerd Muller,FIFA kupitia kwa msemaji wake alikaririwa akisema hakuna anayeweza kuthibitisha uhalali wa Messi na Chitalu kwa sababu FIFA haitunzi rekodi za ligi za ndani zinazosimamiwa na vyama vya soka.
Hata hivyo uchambuzi wa kumaliza suala hilo huenda ukawa na utata kutokana maendeleo ya sayansi na teknolojia kwani itambeba zaidi Messi unaweza kuyapata magoli karibu yote aliyofunga kwa video na kwa mtandao.Je Chitalu utayaona?Hata hivyo FAZ italaumiwa kwa kutotunza vyema kumbukumbu.

Suala lingine linaloibuka hapa ni  kwamba, Je FAZ itategemea utetezi wa watafiti wa historia za michezo kama Muchemba hata mbele ya FIFA mpaka lini? Ikumbukwe Enzi ya uongozi wa Rais wa kwanza wa Zambia Kenneth Kaunda walikuwa na Kikosi hatari kikiwa na Godfreya Chitalu licha ya kushindwa katika fainali dhidi ya Zaire(Congo DRC) lakini hatimaye Zambia imefanikiwa kutwaa ndoo hiyo mwaka 2012 kwa kuifunga Ivory Coast kwa mikwaju ya Penati.

Timu ya Taifa Zambia
Hata kama FIFA watamkubali Chitalu baadhi ya wakosoaji wake wataibua  suala lingine hapa je ubora wa ligi ya Zambia na La Liga Hispania anakocheza Messi na wenzake ni sawa?Watahoji viwango vya timu alizokuwa anacheza nazo pia kwa upande wa Messi hata Record za Guinness na FIFA zaweza kumtambua Messi kwa sababu rekodi zake ni rahisi kupatikana.

Hata hivyo wakosoaji wa Messi katika mafanikio yote aliyowahi kuyapata wanasema atathibitisha ubora wake mbele wachezaji wengine nguli zaidi ulimwenguni kama Pele na Diego Maradona atakapoiwezesha timu yake ya Argentina kupata ubingwa wa kombe la Dunia hadhi ya juu kabisa katika michuano ya FIFA shirikisho la kandanda ulimwenguni.
Rais TFF

Tukirudi Tanzania yetu je tumejipangaje? Endapo tu baadhi ya timu zimediriki kuchezesha wachezaji waliosimamishwa kwa kutumikia kadi nyekundu huku viongozi wake  wakilalamikia kutokumbushwa na TFF? Je  tukihitaji rekodi sahihi zisizo na shaka za kina Jela Mtagwa au Sunday Manara,Kitwana Manara tutazipata kweli au ndo kila mtu ataongea ya kwake.
 Kuanzia  Jumatatu ijayo tutawaletea wasifu wa wachezaji hawa watatu Gerd(Gerhard) Muller,Godfrey Chitalu na Lionel Messi ili pia msomaji wa makala haya uweze kupambanua na kujua utofauti.
Naomba kuwasilisha.................