Mwanamuziki Koffi Olomide wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusu tamasha litakalofanyika Leaders Club Leo Usiku
Mwanamuziki nguli kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Koffi Olomide anatarajiwa kuwasha moto leo katika Ukumbi wa Leaders jiji Dar es Salaam.

Katika mkutano na waandishi wa habari hapo jana katika Ukumbi wa Serena, Kofi aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kupata burudani ya aina yake.

Kwa upande wa Emphraim Mafuru, Mkurugenzi wa masoko Serengeti Breweries amesema kuwa katika msimu wa sikukuu Waafrika wanahitaji burudani ya kiafrika kutoka kwa wanamuziki wa kiafrika na Koffi Olomide ndiye gwiji mwenyewe wa muziki huo.
“Bila shaka mashabiki wetu wanahitaji muziki wa kiafrika huku wakiburudika na kinywaji chenye historia ndefu barani Afrika ambacho ni Bia ya Tusker Lager”, Mafuru alisisitiza.

Koffi Olomide
Antoine Christophe Agbepa Mumba ama Koffi Olomide alizaliwa mwaka 1956 huko Kongo DRC na ni mwanamuziki ambaye amekuwa na mafanikio makubwa katika muziki wa asili ya Kongo kama Soukous ndani na nje ya nchi hiyo ya Kongo. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top