Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh. Shukuru Kawambwa
uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu.
Akitangaza matokeo hayo jijini Dar es salaam waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dk.Shukuru Kawambwa amesema matokeo hayo ya mwaka huu yanaonesha kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 8.8 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana. Amesema kati ya watahaniniwa waliofaulu ,asilimia 50.2 ni wasichana na asilimia 49.8 ni wavulana
Waziri Kawambwa amesema ukilinganisha na mtihani wa mwaka jana,vitendo vya udanganyifu vimepungua ambapo wanafunzi 293 pekee ndio waliofutiwa matokeo kutokana na udanganyifu huku kwa mwaka jana jumla ya wanafunzi 9,736 walibainika kufanya vitendo hivyo.
Waziri Kawambwa ameongeza kuwa jumla ya wanafunzi 3,087 wamefaulu kwa daraja A,wanafunzi 40,683 wamefaulu kwa daraja B huku wanafunzi 222 wakifaulu kwa daraja C.
0 comments:
Post a Comment