Taasisi ya utafiti na tathmini ya rasilimali Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imepanga kufanya maandamano makubwa septemba 22 ili
kupambana na ujangili dhidi ya Tembo ambao unalikabili taifa kwa sasa.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo Profesa Amos Majule
amesema watanzania wanatakiwa kuangalia mwenendo na mustakabali wa TEMBO ambao
wako hatarini kutoweka kutokana na kuuawa kwa wingi.
Profesa Majule amesema jitihada za pamoja
zinahitajika katika kuhakikisha mapambano dhidi ya mauaji ya tembo ambapo
maandamano hayo yatapambwa na kauli mbiu jiunge katika mapambano dhidi ya
wauaji wa tembo.
Mtafiti wa taasishi hiyo Elikana Kalumanga
amesema changamoto kubwa ya tembo kuwa katika hatari ya kutoweka inatokana na
soko la dunia linalohitaji zaidi pembe za ndovu.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment