Wataalam wa tiba ya asili wametakiwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ili kulinda heshima
ya taaluma hiyo katika jamii .
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama cha tiba
asili Tanzania Simba Abdulrahmani Simba na wakati akizungumzia maandalizi ya kuelekea
maadhimisho siku ya tiba asili barani Afrika ambayo yatafanyika kitaifa Agosti
31 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Amesema
kuwa moja katika vigezo vya msingi kwa mtaalam wa tiba asili ni kujisajili kwa
mujibu wa sheria na kuwa na vyeti vinavyowatambulisha katika kazi hiyo.
Amekanusha madai ya baadhi ya watu kuhusisha uganga
wa tiba asili na imani za ushirikina kwamba daktari wa kweli anatakiwa
kuitumikia jamii na si vinginevyo.
Licha ya chama cha waganga wa tiba asili Tanzania
kufanya kazi kwa kushirikiana na serikali na taasisi nyingine kimekuwa na
changamoto ya kupambana na waganga wanaokiuka sheria na taratibu za tiba hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment