Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif na mwenzake wa Marekani Johh Kerry mjini Geneva November 24, 2013 
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif na mwenzake wa Marekani Johh Kerry mjini Geneva November 24, 2013
Maafisa wa Israel wameushutumu vikali mkataba  wa nuklia na Iran uliofikiwa mapema Jumapili mjini Geneva wakisema kuwa mkataba huo kamwe hauzuii Iran kuendelea na juhudi zake za kutengeneza silaha za nuklia.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alishtumu vikali mkataba wa nuklia wa Iran mara tu ulipotangazwa akisema “ huu sio mkataba wa kihistoria, ni kosa la kihistoria.”

Netanyahu alisema dunia inakabiliwa na hatari zaidi kutokana na kile alichoita utawala hatari zaidi duniani  ambao umepiga  hatua kubwa  katika azma yake ya kupata  silaha hatari duniani.

Bw. Netanyahu aliongeza kuwa Israel ina wajibu wa kujilinda kutokana na vitisho vyovyote vile na akaapa kuwa hatakubalia Iran kutengeneza silaha za nuklia.
Iran pamoja na nchi sita sita zenye nguvu duniani zilitangaza kufikiwa mkataba huo wa muda  Jumapili alfajiri baada ya siku nne za majadiliano mazito.

Mkataba huo unailazimu Iran kukubalia wakaguzi wa kimataifa wa silaha za nuklia kukagua viwanda vyake vya nuklia kwa maelewano kuwa ikiwa itatii masharti yote yaliyowekwa,haitawekewa vikwazo vya kiuchumi kwa miezi sita.

Lakini Israel na baadhi ya serikali za Magharibi zinasema zitafanya maamuzi zenyewe juu ya kutumia majeshi kushambulia viwanda vyovyote vile vya nuklia nchini Iran endapo zitagundua  kuwa vipo. 
VOA 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top