Wanajeshi wa DRC
Jeshi la congo linasema kuwa mapigano na waasi wa M23 yamesababisha vifo vya zaidi ya wapiganaji 900 tangu mwezi Mei.

Msemaji wa jeshi Genarali Jean-lucien Bahuma alisema kuwa takriban wanajeshi 200 na zaidi ya wapiganaji 700 waliuawa katika mapigano katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo waanajeshi watatu wa amani wa UN pia waliuawa kwenye makabiliano hayo.

Pia wapiganaji 72 wa Rwanda na wapiganaji 28 wa Uganda waliuawa.

Mwanzoni mwa mwezi huu, waasi wa M23 walitolewa na jeshi la serikali iliyoungwa mkono na kikosi cha wanajeshi wapatao 5000 wa Umoja wa Mataifa lakini serikali ya Congo na waasi walikosa kuelewana kuhusu mpango wa baadae wa amani.

Waasi wa M23 walisitisha vita na kujisalimisha baada ya jeshi la DRC kwa ushirikiano na wanajeshi wa UN kupigwa vita vikali na kuwaondosha katika maeneo waliyokuwa wameyateka.

Maelfu ya wakaazi wa Mashariki mwa DRC walilazimika kukimbilia nchi jirani ya Uganda kutafuta hifadhi wakati kundi hilo lilipokuwa linaendesha uasi wao na hata kuuteka mji wa Goma kwa muda.

Kundi la M23 lilifanya vitendo vya kikatili dhidi ya watu wa Mashariki mwa DRC ikiwemo ubakaji na kuwatumia watoto kama wapiganaji.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top