Rais
wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kutekeleza Ilani
ya uchaguzi ya CCM katika kuimarisha sekta za maendeleo ikiwemo huduma
ya maji safi na salama katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba.
Dk. Shein aliyasema hayo leo kwa nyakati tofauti katika ziara yake ya Kichama katika Wilaya ya Kusini Unguja.
Dk.
Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefanya juhudi kubwa
za kutafuta fedha kwa njia ya mkopo zaidi ya bilioni 64.4 kutoka Benki
ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuimarisha
sekta ya maji pamoja na Tsh. 36 kwa ajili ya miundombinu ya maji hapa
Zanzibar.
Jitihada
zinafanywa katika kuhakikisha tatizo la maji linamalizika katika maeneo
mbali mbali ya Zanzibar likiwemo Jimbo la Makunduchi.
Katika
ziara hiyo, Dk. Shein aliweka jiwe la msingi mradi wa Chama wa maduka
na kupata maelezo pamoja na kukagua ujenzi wa ukumbi mpya wa mikutano
uliopo katika eneo la afisi ya CCM Wilaya ya Kusini Unguja.
Dk.
Shein pia, aliweka jiwe la msingi katika jengo la ushirka wa UWT, Daima
Tupendane. Aidha, alifika Tawi la CCM Mzuri kuangalia ukarabati wa
afisi ya Tawi la CCM na kusalimiana na wanachama wa CCM wa Wadi ya Mzuri
na kutoa kadi za CCM kwa wanachama wapya 203.
Mara
baada ya kuweka jiwe la msingi katika jingo la ushirika wa UWT, Daima
Tupendane, Dk Shein alipongeza juhudi za ushirika huo na kuahidi
kuwasaidia walipofikia katika ujenzi huo pamoja na kuwapa mtaji wa
kuanzisha bekari ya mikate. Dk. Shein alieleza juu ya suala zima la
ajira kwa vijana na jinsi serikali ilivyojipanga juu ya hilo.
Baada
ya hapo Dk. Shein alikagua ukarabati wa Tawi la CCM Bwejuuambapo
alipokelewa kwa shangwe kubwa na kuwapa kai wanachama wapya 186 wakiwemo
vijana na baadae aliwasalimia.
Nae
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali alisema kuwa ziara zake
zimewaonesha njia wanaCCM katika msimamo wa kuimarisha Muungano na vipi
unatakiwa ulindwe na udumishwe sanjari na Mapinduzi matukufu ya Januari
12, 1964.
Akiwa
katika majumuisho ya Mkoa huo baada ya kumaliza ziara yake, Dk. Shein
alisema kuwa uhai wa chama umo katika vikao, na kusifu juhudi
zilizofanywa na viongozi wa chama pamoja na juhudi za utekelezaji wa
Ilani na Sera za CCM na kuupongeza Mkoa huo kwa kingiza wanachama wapya.
Pamoja
na hayo, Dk. Shein aliupongeza Mkoa huo wa Kusini kwa kuendelea kuenzi
na kuitunza historia ya ASP hadi kufikia CCM nakueleza kuwa ziara hiyo
imefana sana.
Aidha,
alieleza kuwa Mapinduzi ya Januari 1964, ndio mkombozi wa nchi na
lazima wafundishwe vijana jinsi Zanzibar ilivyokombolewa na kwa nini
Mapinduzi yametokea. Aidha, alieleza umuhimu wa Muungano na mafanikio
yake yaliopatikana na kusisitiza utadumishwa daima.
Viongozi wa CCM ni lazima wajue kuwa wanajukumu la kuwatumikia wanaCCM il kuweza kuimarisha chama.
Alizma
Mkoa wa Kusini kujitahidi kuimarisha chama na kuhakikisha afisi za
Matawi zinakuwa na nyenzo za kufanyia kazi huku akieleza jinsi
alivyofurahishwa na mashirikiano yaliopo kati ya Wabunge na Wawakilishi
na kusisitiza kuzidisha mashirikiano hayo.
Alieleza
kuwa anafarajika sana kuwaona viongozi wa Majimbo wanakuwa kitu kimoja
na kueleza matumaini yake katika ziara hiyo kwani wameanza vizuri na CCM
ina kasi kubwa.
Uongozi wa Mkoa huo aliwataka kujiandaa katika uchaguzi ujao wa mwaka 2015 na kuhakikisha CCM,inashinda uchaguzi huo.

0 comments:
Post a Comment