LIGI
KUU YAINGIA RAUNDI YA 25
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea katika raundi yake ya 25 kesho (Mei Mosi) kwa
mechi tano zitakazochezwa katika miji ya Dar es Salaam, Turiani, Morogoro na
Mlandizi.
Licha
ya kuwa tayari Yanga imetawazwa kuwa mabingwa wa VPL msimu huu (2012/2013),
mechi dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni
moja kati ya zitakazovuta macho na masikio ya washabiki wa mpira wa miguu
nchini.
Mechi
hiyo namba 172 itachezeshwa na mwamuzi Simon Mberwa kutoka Pwani akisaidiwa na
Said Mnonga na Charles Chambea wote wa Mtwara wakati mwamuzi wa mezani atakiwa
Hashim Abdallah wa Dar es Salaam. Kamishna wa mechi hiyo ni David Lugenge
kutoka Iringa.
Viingilio
katik mechi hiyo itakayoanza saa 10.15 jioni ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya
bluu na kijani, sh. 8,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 kwa VIP C
na B wakati VIP A itakuwa sh. 20,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mchezo.
Mtibwa
Sugar itakuwa mwenyeji wa African Lyon katika mechi namba 170 itakayochezeshwa
na mwamuzi Dominic Nyamisana wa Dodoma kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Turiani
mkoani Morogoro. Nayo Kagera Sugar iliyo katika nafasi ya tatu kwenye msimamo
wa ligi hiyo itakuwa mgeni wa Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro.
Uwanja
wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam na wenye uwezo wa kuchukua
watazamaji 7,000 uko tayari kwa mechi kati ya JKT Ruvu na Tanzania Prisons.
Nayo Ruvu Shooting itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake Mabatini ulioko
Mlandizi, Pwani kuikabili Oljoro JKT kutoka Arusha.
MTANZANIA
APEWA ITC KUCHEZA MSUMBIJI
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC)
kwa mchezaji Yusuf Kunasa kucheza nchini Msumbiji.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu cha Msumbiji (FMF) lilituma maombi TFF kumuombea hati hiyo
Kunasa anayekwenda kujiunga na timu ya Estrela Vermelha da Beira inayocheza
Ligi Kuu nchini humo.
Kunasa
ambaye msimu huu hakuwa na timu (free agent) amejiunga na timu hiyo akiwa
mchezaji wa ridhaa (amateur). Zaidi ya wachezaji kumi kutoka Tanzania hivi sasa
wanacheza katika klabu mbalimbali nchini Msumbiji.
MECHI
YA SIMBA, POLISI MOROGORO YAINGIZA MIL 18/-
Mechi
namba 163 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Aprili 28 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba kuibuka ushindi wa mabao
2-1 dhidi ya Polisi Morogoro imeingiza sh. 18,014,000.
Watazamaji
3,145 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh.
5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh.
3,564,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh.
2,747,898.31.
Kiingilio
cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo
walikuwa 2,841 na kuingiza sh. 14,205,000 wakati idadi ndogo ya washabiki
ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 36 na kuingiza sh.
720,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,812,331.75, tiketi sh.
3,183,890, gharama za mechi sh. 1,087,399.05, Kamati ya Ligi sh. 1,087,399.05,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 543,699.53 na Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 422,877.41.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment