JOSE MOURINHO NIKO TAYARI KULAUMIWA TUKITOLEWA


Kocha wa Timu ya Real Madrid, Jose MourinhoKocha Jose 

Mourinho amechochea moto kwenye mbio za kuwania fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya kwa kusema kuwa yuko tayari kubeba lawama ikiwa klabu yake ya Real Madrid itatupwa nje ya michuano dhidi ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Mechi hiyo itapigwa usiku wa leo ambapo Real Madrid inahitaji ushindi wa magoli 3 – 0 ili kutinga fainali mara baada ya kuangukia pua baada ya kufungwa magoli 4 – 1 katika mechi ya kwanza iliyopigwa Signal Iduna Park huko Ujerumani.

Ushindi wa 4 - 1 mpaka dakika 90 utafanya kuongezwa dakika 30 mshindi asipopatikana changamoto ya mikwaju ya penati itatumika kuamua mbabe wa kutinga fainali ya michuano hiyo.Tayari Jose Mourinho kasema katika soka lolote linawezekana.

Kocha huyo amesema badala ya wachezaji wake kulaumiwa yeye ndiye anastahili kubeba lawama zote ‘katika soka wadau wengi wanahusika katika mafanikio ya timu lakini pindi timu hiyo ikifanya vibaya lawama zote anatakiwa kuzibeba kocha’alisema kocha Mourinho.

Mario Goetze


Robert Lewandovsky
 Licha ya tishio la kuondoka kwa wachezaji wake mahiri Mario Goetze na Robert Lewandovsky,kocha Mourinho amesema anaamini Dortmund wataendelea kuwa imara na kuwapata wachezaji mbadala wa nafasi hizo.

Dortmund ilishinda taji la ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 1997 huku Real Madrid ikishinda taji hilo mwaka 2002.

Mahasimu wa Real Madrid FC Barcelona watakuwa na kibarua pevu cha kurejesha matumaini ya kutinga fainali itakaposhuka ugani siku ya Jumatano usiku dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani huku ikiwa na kumbukumbu ya kuchabangwa magoli 4 – 0 katika dimba la Allianz Arena huko Munich.
BARCA watahitaji ushindi wa magoli 5 - 0 ili kufuzu fainali ushindi wa magoli 4 - 0 katika dakika 90 utawapeleka dakika 30 za nyongeza ikishindikana hapo ni changamoto ya mikwaju ya penati kuamua mshindi.Lionel Messi na Xavi Hernandez wamekiri ugumu uliopo katika kubadili matokeo hayo.
NI LIONEL MESSI TU ATAKAYETUBEBA-BARCA
Lionel Mess
Xavi Hernandez
Wakati timu ya Barcelona ya Hispania  ikitaraji kushuka ugani siku ya Jumatano kupambana na Bayern Munich ya Ujerumani katika mechi ya marudiano ligi ya mabingwa Ulaya imekiri kuwa kutinga fainali kunategemea ubora wa Messi siku hiyo.

Katika mechi ya awali miamba hiyo ya Catalunya iliambulia kichapo cha magoli 4 – 0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa dimba la Allianz Arena.

Kocha msaidizi wa BARCA Jordi Roura amesema afya ya mchezaji huyo imekuwa ikiimarika lakini anaamini atakuwa fiti kwa mchezo huo utakaochezwa katika uwanja wao wa nyumba NOU CAMP.

‘messi ni mchezaji bora duniani hivyo asipokuwepo dimbani utaona tofauti na akiwepo dimbani utajua utofauti wake’.

Kutokuwa fiti kwa asilimia 100 kwa Messi katika mchezo uliopita dhidi ya Bayern Munich ni miongoni mwa kinga kwa makocha wa Barcelona kupoteza mechi hiyo.

BARCA watahitaji ushindi wa magoli 5 - 0 ili kufuzu fainali ushindi wa magoli 4 - 0 katika dakika 90 utawapeleka dakika 30 za nyongeza ikishindikana hapo ni changamoto ya mikwaju ya penati kuamua mshindi.

Lionel Messi na Xavi Hernandez wamekiri ugumu uliopo katika kubadili matokeo hayo.

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top