Zitto Kabwe
ALIYEKUWA Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anatarajia kufanya
mkutano mkubwa wa hadhara jimboni mwake kesho. Zitto anatarajia kujibu
mashambulizi yaliyoelekezwa kwake na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk.
Wilbrod Slaa alipofanya ziara ya kutembelea mkoa huo hivi karibuni.
Akiwa mkoani humo, Dk. Slaa alisema wafuasi wote wanaopinga kuvuliwa nyadhifa, Zitto wanapaswa kujiondoa ndani ya chama wenyewe.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Muhange wilayani Kakonkoo jana, Dk. Slaa alisema uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kumvua nyadhifa zote Zitto utaendelea kuheshimiwa.
“Nimesikia kilio chenu kila mmoja, anauliza Zitto yuko wapi, napenda kuwaambia uamuzi wa Kamati Kuu utaendelea kuheshimiwa ndugu zangu.
“Kama kuna mtu ambaye anaona Zitto ameonewa nasema yuko huru kuondoka ndani ya Chadema, ili akaungane naye kuanzisha harakati nyingine…chama hiki kinafuata sheria, taratibu na kanuni zilizopo.
“Nawaambia kama kuna kundi la watu liliingia kwa sababu ya Zitto, nawashauri bila kinyongo chochote milango iko wazi kwao kutoka….chama hakifi kwa sababu mtu mmoja hayupo,” alisema, Dk. Slaa.
Alisema CHADEMA hakitakufa kutokana na vurugu au kampeni chafu zinazofanywa na watu au vyombo vya dola.
“Nawahakikishia CHADEMA haiogopi kiongozi hata mmoja, awe Freeman Mbowe (mwenyekiti), Slaa (Katibu) atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu zetu, sisi tunachoogopa siku zote ni katiba ya chama,” alisema Mbowe.
Dk. Slaa alisema hayo baada ya vijana wanne waliokuwa na mabango kuvamia mkutano wake, ambapo polisi walilazimika kuwaondoa eneo la mkutano.
Habari za uhakika zilizopatikana kutoka mkoani Kigoma, zinasema Zitto atawasili kesho asubuhi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma ambako atapokelewa na wafuasi wake.
Akizungumza na RAI jana, Katibu Mwenezi wa chama hicho Mkoa wa Kigoma, Hajji Mbaga alisema baada ya kupokelewa atakwenda katika Kijiji cha Mwandiga ambako atahutubia mkutano wa hadhara.
Alisema katika mkutano huo, Zitto atazungumzia mambo mbalimbali yaliyojitokeza, ikiwa ni pamoja na kuvuliwa nyadhifa zote za uongozi na Kamati Kuu ya chama hicho mwezi uliopita.
“Tunatarajia kumpokea mbunge wetu hapa, kisha atakwenda jimboni kuzungumza na wananchi kuhusu mambo mbalimbali ambayo yamejitokeza katika siku za karibuni.
“Ni wazi wananchi watapewa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kama unavyojua, Dk. Slaa alikuwepo hapa kwa wiki nzima na mlisikia mambo aliyosema, sasa watu wetu wana kiu ya kupata majibu ya msingi,” alisema Mbaga.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:
Post a Comment