Katibu mkuu wa UVCCM, Martine Shigella, leo amezungumza na wandishi wa habari ambapo amesema kuwa mgambo wa CHADEMA ni kinyume na sheria.
1.kuanzishwa kwa REDBRIGED ya chadema hakukubaliki, chadema lazima watofautishe kati ya vijana wa CCM ambao wanapewa mafunzo ya ukakamavu juu ya chama katika kueneza sera na kuandaliwa kama viongozi wa baadae na kikundi cha kijeshi kinachoanzishwa na wao kwa maana wanaosema ya kujilinda DHIDI YA POLISI


CCM haina kikundi cha kujilinda dhidi ya polisi au wanajeshi. UVCCM inavikundi kwa ajili ya ukakamavu wa vijana wake,je chadema hawatakuwa na haja ya kuwa na askar polisi kwenye mikutano yao?  so hilo tunalilaani na hatuliungi mkono


2.Tunataka vijana wetu toka kwenye mashina matawi ,kata na wilaya washiriki vyema kuwaaambia wajumbe wa mabaraza ya katiba maoni wanayoona yanafaa kwenye katiba mpya.


Hatuungi mkono ujio wa serikali tatu , gharama za serikali hizo ni mzigo kwa watanzania lakini pia mchakato wa kuleta serikali ya tatu haukubaliki,unawezaje leo upate mtoto wakati mzazi mmoja haujamtafuta?


Inamana Zanzibar wana katiba yao, Bara unasema hawana katiba yao eti itakuja baadae?


Walipaswa kwanza waje na mapendekezo ya rasimu ya jinsi serikali ya Zanzibar inavyopaswa kuwa katika serikali ya muungano.


Pili waje na mapendekezo ya katiba ya jinsi Serikali ya Bara itakavyokuwa.


Na mwisho waje na rasimu ya serikali ya muungano ili kila upande ujijue na si tuanze na serikali ya muungano halafu eti Bara tuje tujijue baadae.


PILI katika huo mchakato wa katiba kuna mambo mengi ambayo hayapo sawa,


Mfano eti wanataka vijana wagombee ubunge wakiwa na umri wa miaka 25.


Hii si sawa, mimi nilidhani wangesema kwa kuwa vijana wana haki ya kupiga kura wakiwa na miaka 18, basi wawe na haki ya kugombea ubunge pia wakiwa na miaka hiyo hiyo.

Hao wajumbe wa katiba walipata uteuzi wa kuwa mabalozi nje ya nchi wakiwa na miaka 18 mfano Dk Salim A. Salim.

Sasa wanataka kuwachelewesha tu vijana ambao mtakubaliana nami kuwa sasa wamekua kiakili zaidi kuliko vijana wa wakati ule wa analojia na wakati huu wa dijitali.


Na kwa kuwa hakuna kijana aliyegombea ubunge akiwa na chini ya maiaka 25 ameonyesha kushindwa majukumu yake basi tunaomba umri ubaki ule ule wa awali wa miaka21 au uwe miaka 18.


3. Mwisho kutakuwa na uchaguzi wa chipukizi taifa mwaka huu 2013 na fomu zinaanza kutolewa tar 5/7-30/07/2013 fomu zitatolewa mikoani,UVCCM zanzibar na UVCCM makao makuu zanzibar


Nafasi zinazogombea ni:


1.mwenyekiti wa chipukizi taifa nafasi 1

2.makamu mwenyekiti taifa nafasi 1

3.wajumbe wa wili wa baraza kuu taifa kutoka chipukizi nafasi moja bara na moja zanznibar

4. wajumbe wanne wakamati ya uendeshaji taifa wawili toka zanznibar na wa wili toka bara

5.wajumbe watatu wa mkutano mkuu wa UVCCM taifa chipukizi kwenda mkutano mkuu wa UVCCM Taifa ,nafasi mbili toka bara na nafasi moja toka zanzibar.
Chanzo: Ccmblog
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top