Serikali ya marekani imetoa nafasi maalum za mafunzo kwa wanafunzi vyuo vikuu nchini kwenda kusoma masuala ya kilimo nchini Marekani.

Mwakilishi wa shirika la misaada la Marekani Tomm Hubgood amesema katika kuboresha uhusiano baina ya Tanzania na marekani na kuisaidia Tanzania katika kukuza sekta ya kilimo hapa nchini.

Bwana Hubgood  amesema kuwa Lengo kubwa la mradi huo amesema ni kuwajengea uwezo wataalam hapa nchi na kuhakikisha wanaboresha usalama wa chakula kwa nchi ya Tanzania. 

 Mtalaam wa Kilimo Emmanuel Mgonja kutoka wizara ya kilimo na chakula ambaye yuko masomoni nchini Marekani amesema nchi zilizoendelea zinathamini tafiti zinazohusu  masuala ya kilimo ambapo zikifanyiwa kazi zinaleta tija katika sekta husika.

Nao wataalam wanaotarajia  kusomea masuala ya kilimo nchini Marekani wamesema watatumia ujuzi waliupataa kwa manufaa ya wananchi katika jitihada za kuendeleza kilimo hapa nchini.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top