Mamia ya watu wanaaminika kufa wakati wa mapigano
baina ya majeshi ya yanayomuunga mkono rais wa Sudan Kusini na yale
yanayomuunga mkono makamu wa rais, maafisa wa Umoja wa Mataifa waliopo
Sudan Kusini wamesema baada ya kunukuu ripoti ambayo bado
haijathibitishwa.
Wanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa wamesema
wameambiwa na vyanzo vya habari katika mji wa Juba kwamba idadi ya watu
waliokufa wanaweza kufikia 400 hadi 500.
Sudan Kusini imekuwa na mapigano ya siku mbili kufuatia taarifa kwamba kulikuwa na jaribio la kumpindua rais Salva Kiir.
Mwanasiasa wa upinzani aliyeko uhamishoni Riek Machar amekana madai ya serikali kuwa alijaribu kufanya jaribio hilo.
"Kilichotokea Juba ni kutokuelewana na
mgawanyiko baina ya vikosi vya ulinzi vya rais, sio jaribio la
mapinduzi," aliiambia Sudan Tribuni, tovuti yenye makao yake Paris
katika mahojiano yaliyochapishwa siku ya jumatano.
Bwana Machar Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan
Kusini ambaye aliondolewa na rais Kiir mwezi Julai, amesema hana taarifa
wala hausiki kwa namna yoyote na jaribio hilo la mapinduzi.
Rais wa Sudan Kusin Salva Kiir amesema kundi la
wanajeshi wanaomuunga mkono makamu wa rais Machar walikuwa wakijaribu
kujitwalia madaraka kwa kwa nguvu siku ya Jumapilil usiku, lakini
walishindwa.
Wakati mapigano yanaendelea siku ya jumatatu na
jumanne, serikali imesema wanasiasa kumi maarufu akiwemo waziri wa
zamani wa fedha, wametiwa mbaroni.
Taarifa za mapigano hayo zimefika kwenye baraza
la kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York siku ya jumanne, ambapo
limesema mapigano hayo yanaweza kuwa mapingano ya kikabila.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment