Moja ya majeruhi katika mlipuko uliotokea nchini Somalia
Madktari raia wa Syria na wa jamii ya kisomali
wameuawa kwa kupigwa risasi baada ya kufanyika shambulizi karibu na mji
mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia BBC kuwa watu wenye silaha walishambulia gari lililokua likielekea katika hospitali moja.
Walinzi wao wawili pia waliuawa katika shambulio hilo, huku daktari mmoja wa Syria na mwingine wa Somalia wakijeruhiwa .
Wanamgambo wa kiislamu, Al Shabaab wamekuwa
wakisabisha hali ya usalama kuzorota nchini Somalia, hata hivyo
haijathibitika ni nani anayehusika na shambulio hilo.
Madaktari wa Syria wanaelezwa kuwa walikua nchini Somalia kwa ajili ya shughuli za kutoa misaada.
Mwandishi wa BBC ameripoti kuwa shambulio hilo
lilitokea katika wilaya ya Siinka Dheer inayodhibitiwa na Serikali, eneo
lililo kusini mwa Mogadishu.
Madaktari waliojeruhiwa wako hospitalini
wakipatiwa matibabu mjini Mogadishu, halikadhalika miili ya watu sita
waliouawa katika shambulio hilo imefikishwa hospitalini.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment