Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwanzilishi na Afisa Mtendaji
Mkuu wa CEO Clubs Network, Bwana Tareq Ahmed Nizami, mwandaaji mwenza wa
Mkutano wa Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia, 'The
Africa -Middle East-Asia' unaofanyika katika Hoteli ya Atlantis The
Palm, huko Dubai katika Jamhuri ya Falme za Kiarabu (UAE), tarehe
16.12.2013. Mwandaaji mwingine wa mkutano huo ni Kituo cha Maendeleo ya
Kiuchumi na Uongozi (CELD).
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Penehupifo Pohamba, Mke
wa Rais wa Namibia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku tatu wa
wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika Dubai
kuanzia tarehe 16.12.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Balozi wa Tanzania katika
nchi za Falme ya Kiarabu (UAE) wakati wa sherehe za ufunguzi wa Mkutano
wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika katika
hoteli ya Atlantis The Palm iliyopo Dubai, Jamhuri ya Falme za Kiarabu
tarehe 16.12.2013. Kushoto kwa Mama Salma ni Mke wa Rais wa Namibia Mama
Penehupifo Pohamba, na wa kwanza ni Mshauri Maalum wa Mama Pohamba
Mchungaji Justina Hilukiluah na wa mwanzo kushoto no Bwana Tariq Nizami,
Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa CEO Clubs Network.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasilisha mada ya Elimu: Key to the
Future of Women in Emerging Economies, kwenye mkutano wa siku tatu wa
Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unaofanyika huko Dubai
tarehe 16.12.2013.
Mke
wa Rais wa Namibia Mama Penehupifo Pohamba akimpongeza Mke wa Rais,
Mama Salma Kikwete baada ya kutoa mada iliyosisimua wajumbe wa Mkutano
wa Wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia unafanyika jijini
Dubai, Jamhuri ya Falme aza Kiarabu tarehe 16.12.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na Mheshimiwa Margaret Zziwa, Spika wa
Bunge la Afrika Mashariki. Viongozi hao ni miongoni mwa viongozi
wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia wanaohudhuria mkutano
wa siku tatu huko Dubai.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Dr. Angela Moore,
Balozi wa Heshima kutoka Jimbo la Georgia, nchini Marekani wakati wa
mkutano wa wanawake kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia huko Dubai
tarehe 16.12.2013. PICHA NA JOHN LUKUWI
0 comments:
Post a Comment