Mkurugenzi mtendaji wa LHRC, DK. Hellen Kijo Bisimba.
 
Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC kimemshauri waziri mkuu Mizengo Pinda kuwaomba radhi wananchi kutokana kauli aliyoitoa bungeni siku ya alhamisi inayodaiwa kuwachanganya wananchi.

Alhamisi wiki hii wakati akijibu maswali ya papo kwa papo bungeni mjini Dodoma waziri mkuu alinukuliwa akisema jeshi la polisi litaendelea kutumia shuruti kwa yeyote atakayekaidi  amri zinazotolewa kwa mujibu wa sheria.

Mkurugenzi mtendaji wa LHRC Dakta Hellen Kijo Bisimba amesema Wananchi wanaamini yeye ndiye mtendaji mkuu wa serikali hivyo anatakiwa kusimamia sheria na kanuni za nchi.

Mkurugenzi huyo amesema hakuna mtu wala kiongozi ambaye yuko juu ya  sheria hivyo kauli ambayo inachochea watu kujichukulia sheria mikononi hazifai kutolewa na viongozi na watendaji wa serikali.

Dakta Kijo Bisimba amesema  siyo mara ya kwanza kwa waziri mkuu Mizengo Pinda kutoa kauli zenye utata kwani amewahi kutoa kauli kama hizo wakati wa mauaji ya albino na wakati mgomo wa madaktari kauli ambazo ziliiweka jamii katika mtazamo tofauti.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top