MAGARI mawili  kutoka kampuni ya Flying Cargo ya Arusha na Simba Trucking leo alasiri yamefanikiwa kuinasua ndege ya shirika la ndege la Ethiopia, Boeing 767 iliyokuwa imenasa katika tope kwenye uwanja wa ndege wa Arusha.
 
Ndege hiyo kubwa ambayo haistahili kutua katika uwanja huo kutokana na ukubwa wake, ilitua jana katika mazingira ya kutatanisha na kuzua hofu kubwa.
 
Magari hayo mawili  yenye winchi T.897 APE na T. 958 AKS yalianza kazi hiyo saa 8.10 na kuiweka katika eneo la lami saa 9.02.
 
Hata hivyo kabla ya kuvutwa ilikaguliwa na wakaguzi sita  wa Ndege kutoka nchini Ethiopia na wawili wa Tanzania.
 
Ndege hiyo itakaguliwa tena na huenda ikaruka kesho.
 
Ndege hiyo ilikuwa inatoka Addis Ababa Ethiopia na ilikuwa itue katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) lakini rubani alilazimika kutua katika uwanja wa Arusha huku ndege hiyo ikiwa na abiria 213.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top