Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta 
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya ICC amewataka majaji wa mahakama hiyo kuchelewesha kesi ya Rais Uhuru Kenyatta ili apate ushahidi zaidi.
Katika taarifa Alhamis, Bensouda alisema amepoteza mashahidi wawili muhimu na kwa hiyo anaamini kesi dhidi ya rais Kenyatta haitimizi malengo ya viwango vya juu vya ushahidi ambayo sharti  yawepo ili kuweza kuendelea na kesi.

 Alisema anahitaji muda zaidi kutafuta ushahidi zaidi na kuutathmini kubaini ikiwa unafikia vigezo vya mahakama hiyo kuweza kutumika katika kesi dhidi ya rais huyo wa Kenya.

Mwendesha mashtaka huyo anasema shahidi mmoja amesema hana nia tena ya kutoa ushahidi dhidi ya Bw. Kenyatta huku mwingine akisema kuwa ushahidi aliotoa mwanzo ulikuwa wa uwongo.

 Kesi dhidi ya Naibu rais wa Kenya Bw. William Ruto ilianza Septemba na ya bw. Kenyatta ilitazamiwa kuanza Februari 5 mwakani.

Wote wanatuhumiwa kuhusika katika uchochezi wa ghasia zenye maafa zilizofuata baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka wa 2007 na mapema 2008. 
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top