Thamsanqa Jantjie, mkalimani wa lugha ya ishara
Mkalimani wa lugha ya ishara katika siku ya mazishi ya kitaifa, ya aliyekuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, amelazwa katika hospitali ya wagonjwa wa magonjwa ya akili.

Mkalimani huyo anashutumiwa kutoa ishara ambazo hazikuendana na kile kilichokuwa kikiongelewa.

Thamsanqa Jantjie "anaweza kuwa na matatizo", amekaririwa mke wake Siziwe akisema hayo.

Wataalam wa lugha ya ishara wamemshutumu kwa kutoa tafsiri potofu wakati viongozi mbalimbali wakitoa hotuba zao kwenye mazishi ya kitaifa ya Bwana Nelson Mandela wiki iliyopita.

Bwana Jantjie amesema aliumwa ghafla ugonjwa wa schizophrenia na amesisitiza kuwa alikuwa ni mkalimani mwenye ujuzi wa kazi hiyo.

Chama tawala cha African National Congress, ANC, amesema imekuwa ikimtumia Bwana Jantjie kama mkalimani wa lugha ya ishara katika matukio kadha siku za nyuma na hakuwahi kulalamikiwa kuhusiana na huduma yake, kwa upande wa ujuzi au maradhi yoyote.

Bwana Mandela alifariki dunia tarehe 5 Desemba mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95 na kuzikwa Jumapili.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top