Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kata ya
Mwandoya, kijiji cha Mandoya tarafa ya Kisesa ambapo Katibu Mkuu alipata
maelezo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maendeleo ya hatua za awali za
ujenzi wa daraja la Mongobakama ambalo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani
ya uchaguzi ya CCM.
Katibu Mkuu wa
CCM akipokelewa na umati wa wakazi wa kijiji cha Mwasengela ambao kwa ni
nadra kupata viongozi wa kitaifa kwenye kijiji chao.
Mkuu wa Wilaya
ya Meatu Rosemary Kirigini akisalimia wakazi wa kata ya Mwasengela
wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana alihutubia.
Mbunge wa Kisesa
Ndugu Luhaga Mpina akihutubia wakazi ya kata ya Mwasengela kwenye
mkutano wa hadhara ambao mgeni wa heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa kata ya Mwasengela ambapo yupo
kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mkoani
Simiyu .
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na aliyekuwa mgombea wa
udiwani kwa tiketi ya TLP lakini sasa amejiunga rasmi na Chama Cha
Mapinduzi Zunzu Ndatulu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
Mwasengela.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akihutubia wakazi wa kata
ya Mwangesela wilayani Meatu mkoani Simiyu ambapo aliwasifu wakazi wa
kata hiyo kwa kuichagua CCM na kupata viongozi wanaoleta maendeleo.
Mbunge wa Kisesa
Luhaga Mpina akiwatambulisha wazazi wake kwenye mkutano wa hadhara
ambapo aliwaambia wananchi ilimchukua miezi mitatu kukubaliwa kwa ombi
lake la kutaka kugombea ubunge jimboni kwake.
Chifu Kilabanja Abdulrahman Kinana akiwaaga wakazi wa kata ya Mwasengela baada ya kumaliza Mkutano wa hadhara.
Sehemu ya umati
uliofika kwenye mkutano wa hadhara kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mikoa mitatu ambapo
kwa sasa yupo mkoani Simiyu na atamalizia mkoa wa Mara, tayari Katibu
Mkuu ameshamaliza ziara ya mkoa wa Shinyanga na kuleta neema kwa
wakulima wa pamba na wafugaji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na mbunge wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina na wazazi wa mbunge huyo mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka mawaziri
husika kutatua kero za wananchi baada ya watendaji wa chini kushindwa
kufanya kazi zao, alisema sasa baadhi ya watendaji wamegeuza kero za
wananchi mitaji na kuwachangisha pesa nyingi hasa wafugaji.
Akihutubia
wakazi wa kata ya Mwasengela alisema mawaziri lazima wachukue jukumu la
moja kwa moja kutatua matatizo ya wananchi, alisema wafugaji wa kata ya
Mwasengela wamekuwa wakibughudhiwa na watu wa hifadhi ya Maswa kupita
kiasi ambapo alisema sheria nyingine ziangaliwe upya kwa vile zinaweza zikawa zimepitwa
na wakati hivyo ni vyema zikarekebishwa.
CCMblog
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment