Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mh. John Mnyika
Mbunge wa ubungo John Mnyika ameitaka serikali kutekekeleza kwa vitendo ahadi mbalimbali kwa wananchi ikiwemo namna ambavyo rasilimali za nchi zitakavyotumika

Akizungumza jijini bwana Mnyika amesema maandamano yaliyofanywa jana na wananchi wa Mtwara wakipinga gesi kutoka mkoani kusafirishwa kwenda jijini Dar es salaam ni ishara kuwa bado rasilimali za nchi haziwanufaishi walengwa

Amesema maandamano hayo yangeweza kuepukwa endapo mkataba kati ya serikali na wawekezaji wa mradi huo wa gesi ungewekwa wazi ili wananchi waone namna watakavyonufaika

Ameongeza kuwa mikataba mingi ambayo ipo ukiwemo ule wa mradi wa gesi ya Songosongo inalenga kuwanufaisha wachache ambao amewaita ni viongozi walafi na wenye uchu wa kujilimbikizia mali

Mbunge huyo amesema kwa hatua ambayo mradi huo umefikia ni vyema serikali ikaangalia upya uwezekano wa kuupitia upya huku akisema suluhu ya kudumu ya mikataba hiyo ni kurekebisha sera ya nishati
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top