Waziri wa Nishati na madini Mheshimiwa Prof. Sospeter Mhongo
 Wakazi wa  jiji  la Dar es Salaam wamelilalamikia shirika la ugavi wa umeme nchini TANESCO kwa kile kinachodaiwa kuendelea kwa mgao wa kimya kimya wa umeme katika baadhi ya maeneo.

Wakazi hao wamesema kitendo cha TANESCO kukata umeme  bila taarifa kinawasababishia hasara kila siku kwani wengine wanategemea umeme kwa kiasi kikubwa katika kuendesha shughuli zao.

Wamesema tatizo hilo linaathiri biashara zao za  vinywaji baridi,saluni,pamoja na viwanda vidogo vidogo ambavyo nishati ya umeme ni muhimu zaidi kwa uzalishaji mali.

Juhudi za kuutafuta uongozi wa shirika hilo kuzungumzia malalamiko hayo bado zinaendelea

TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top