Wananchi wa kijiji cha Zinga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wameunda kamati ya ufuatiliaji wa suala la mgogoro wa
ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 10 ili kufika kwa mkuu wa mkoa Pwani ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.
Wananchi hao
wamefikia hatua hiyo kufuatia taarifa ya kupotea kwa faili la mgogoro huo wa
ardhi yenye zaidi ya ekari 800 na
kuzusha hali ya wasiwasi miongoni mwa wananchi hao.
Hivi
karibuni wananchi wa Zinga waliwapa
Viongozi wa kijiji hicho siku saba kwa
ajili ya kuhakikisha wanatoa mrejesho wa mgogoro huo ambapo walipoketi idara ya ardhi wilayani iliketi na kamati ya
ufuatiliaji na kugundua dosari hiyo.
Hata hivyo Mkurugenzi
wa Bagamoyo bwana Samweli Sarianga amekiri kuwepo mgogoro
lakini amekanusha taarifa za kupotea kwa
vielelezo vya ardhi katika eneo la Zinga-Matunda Farm na kuongeza kuwa halmashauri
imeunda kamati juu ya sula hilo .
Migogoro ya
ardhi imekuwa ikiongezeka siku hadi katika maeneo mbalimbali hapa nchini hivyo
serikali na wadau wa maendeleo hawana budi kutoa elimu juu ya
masuala ya sheria ya ardhi ili kupunguza migogoro hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment