Kikosi cha Simba |
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya
mabingwa barani Afrika, Simba leo wamevutwa sharubu baada ya kuchapwa magoli 3 – 0 dhidi ya Tusker ya
Kenya katika mchezo wa kimataifa wa Kirafiki.
Mechi hiyo imepigwa katika dimba la Taifa Dar es
Salaam wageni waligeuka kuwa wenyeji katika dimba hilo baada ya kutandaza
kandanda safi na kuwanyuka wekundu hao wa
Msimbazi ,mpaka mapumziko Tusker walikuwa mbele kwa magoli 2 – 0 magoli
yaliyofungwa na Jesse Were.
Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ya
wachezaji lakini waswahili wasemavyo siku ya kufa nyani miti yote huteleza basi
WANA LUNYASI walijikuta wakipigwa mweleka kwa kupachikwa goli la 3 likifungwa na Fredrick Onyango.
Kipigo hicho kimewasononesha sana mashabiki wa
Simba huku wenzao wa Yanga wakiwakejeli karibu muda wote wa mchezo hasa baada
ya wao pia kuzomewa siku Yanga ilipochapwa kwa goli 1 – 0 dhidi ya Tusker katika mechi ya kirafiki.
0 comments:
Post a Comment