Wakati uongozi wa Simba ukisema hautambui mkutano ulioitishwa na baadhi wanachama wa klabu hiyo,kwa kile kinachodaiwa kutofuata kwa misingi ya katiba,kundi linaloupinga uongozi limesema mkutano utafanyika Desemba 30 kama ulivyopangwa.
Wawakilishi wa kundi hilo Ally Msele na Mzee Said Mfaume wamesema mkutano wao utafanyika ukumbi wa  hoteli ya Travertine Magomeni ili kujadili masuala yanaoihusu Simba hususani kuelekea mzunguko wa pili ligi kuu Tanzania bara.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage alikaririwa na duru za spoti mwanzoni mwa wiki hii kuwa mkutano unaodaiwa kuwa wa  dharula hauna baraka yoyote na una malengo ya kuvuruga amani na mshikamano miongoni mwa wanachama,wapenzi na mashabiki wa timu hiyo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

0 comments:

 
Top